Exodus 34:29-32

29 aMusa alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa uking’aa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana. 30Haruni na Waisraeli wote walipomwona Musa, kuwa uso wake unang’aa, waliogopa kumkaribia. 31 bLakini Musa akawaita, kwa hiyo Haruni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. 32 cBaadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.

Copyright information for SwhKC